top of page

MBB NI NINI?

KARIBUNI kwenye Masomo Bunifu ya Biblia

Masomo Bunifu ya Biblia yalitungwa katika nchi ya Indonesia wakati waandishi wakiyafundisha kwa watoto na vijana wa madhehebu mbalimbali. Hivyo masomo haya mwanzoni yaliandikwa katika lugha ya kiindonesia, kupangwa kwa muhtasari wa miaka minane na hivyo kufaa kwa watoto wa umri wa miaka 4-11. Masomo haya yametolewa pamoja  na zana za kufundishia zilizobuniwa kwa kutumia aina mbalimbali. Hivyo kitabu kinaitwa Masomo Bunifu ya Biblia.

Siku hizi masomo haya yameenea katika nchi nyingi za Asia, pia katika nchi moja Afrika Kaskazini, na kupitia toleo la Kiswahili yameifikia Tanzania na nchi jirani zinazotumia lugha hii.

Toleo la kiswahili linawafaa watoto wa Shule ya Jumapili, Chekechea na Shule ya msingi wenye umri wa miaka 4 - 12  na limeandaliwa kuwafundisha watoto katika rika tatu tofauti.

Masomo haya yalijaribiwa na walimu mbalimbali wa Shule ya Jumapili wanaoishi Tanzania.Walitoa  ushauri hapa na pale ili kuweza kuyaboresha kwa ajili ya mazingira ya watoto wa Tanzania na ya nchi jirani.

 

Masomo Bunifu ya Biblia  yalitungwa kwa mpangilio rahisi na yanatumia mbinu bunifu za ufundishaji pamoja na picha  mbalimbali zinazowafaa watoto wa rika tofauti.

 

Masomo Bunifu ya Biblia yaliandikwa juu ya msingi wa upendo na kujitoa kwa ajili ya kizazi kikubwa cha watoto wanaoishi katikati yetu  na wakiwa  na thamani kubwa, lakini mara nyingi kutowajali kulingana na mapenzi ya Mungu. Kuna  nchi, ambazo watoto hudharauliwa na kukandamizwa na ni marufuku kuwafundisha watoto habari za uzima katika Yesu.  Lakini Yesu Kristo alituagiza tuyafundishe mataifa yote wakiwemo watoto kuyashika yote yaliyoamriwa.

​

​​

bottom of page