KARIBUNI KWA
MASOMO BUNIFU YA BIBLIA
SEMINA
Masomo Bunifu ya Biblia
yanatumika vizuri kupitia semina na warsha
Walimu wa watoto na watoto wenyewe watafaidika sana ikiwa Masomo Bunifu ya Biblia yataeleweka na kutambuliwa. Tunaendesha semina na warsha ili kuwawezesha walimu kupata uwezo huu. Semina zinaweza kupangwa kwa muda wa siku mbili hadi nne, zipo za aina mbili tofauti.
Kozi ya msingi:
- Kanuni za Kibiblia za kuwafundisha watoto
- Kuwajua watoto tunaowafundisha (Saikolojia ya watoto)
- Mbinu za ufundishaji
- „Demo-lessons“ – wanasemina wanamtazama mwalimu anavyowafundisha watoto na watafundisha wenyewe wakitumia Masomo Bunifu ya Biblia
- Watajifunza namna ya kutengeneza zana za kufundishia
Warsha ya wawezeshaji wa walimu wa Masomo Bunifu ya Biblia (ToT)
- Mungu, Yesu na Roho Mtakatifu kama walimu
- Mbinu za na namna ya kutambulisha muhtasari ya MBB na kuwafundisha walimu wengine.
- Mazoezi darasani
- Baada ya ToT wawezeshaji watafundisha kozi ya msingi ya MBB wakiongozwa na wawezeshaji wao.
Namna ya kupata semina?
- Tuma e-mail na eleza mahitaji ya kanisa / shirika lako, wahusika watakutumia maelezo zaidi.
- Angalia kwenye orodha ya semina zilizopangwa tayari na wasiliana nasi. Labda kuna nafasi kujiunga pale.